Je unajua ni kwanini ule samaki zaidi kuliko nyama? Hizi hapa sababu kumi

“As soon as I get home, all I want to eat is seafood.”

Sato, kibua,tasi, nguru, perege, sangara, migebuka, changu, kolekole, nguru haya ni baadhi tu ya majina ya aina mbalimbali za samaki hasa zinazopatikana hapa kwetu Tanzania . Je wewe unapenda aina ipi tuambie kwenye comment chini.

Samaki ni chakula chenye utajiri mkubwa wa virutubisho vingi ambavyo vinasaidia ubongo, mwili wako, na hata afya ya ngozi yako. Hizi ni sababu 10 za kutumia vyakula hivi muhimu.

Samaki ni chakula kimojawapo ambacho kina faida kubwa ya protini. Kina utajiri mkubwa wa virutubisho kama omega – 3 fatty acids na ni chanzo kikubwa cha protini kitakochosaidia mwili wako na kuimarisha misuli. Samaki pia inaimarisha ini, mifupa ya kiuno, ubongo, na hata namna unavyotakiwa kupata usingizi wa kutosha. Hivyo hakikisha unatumia chakula hichi muhimu kwa afya nzuri. Twende pamoja kujua faida hizi muhimu kwa afya yako na familia yako;

Kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo Kupitia jarida moja la afya imeelezwa kwamba ulaji wa samaki unasaidia sana kupunguza mtu kupatwa na mshtuko wa moyo na magonjwa mengine yatokanayo na moyo. Samaki ina kiwango kikubwa cha asidi ya omega – 3 fatty acids ambayo inaweza kupunguza inflammation – kuharibika kwa tishu za mwili, inalinda moyo na kukuondolea magonjwa mengine hatarishi.

Kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa ubongo kama Alzheimer’s. Samaki pia ni muhimu sana kwa afya yako ya ubongo. Kula vyakula hivi vitokanavyo na zao la bahari kunapunguza sana hatari ya kupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, uwezo mdogo wa kufikiri na kuua seli za ubongo ambao kitaalamu unajulikana kama Alzheimer’s. Uchunguzi wa wataalamu wa afya unaonyesha kwamba wale wanaokula samaki mara kwa mara wanapata faida ya kupunguza kuchoka kwa ubongo.

Kupunguza kupata msongo wa mawazo Samaki pia na vyakula vingine vya jamii hii vinasaidia sana afya ya akili(mental health) , mafuta ya samaki yanasaidia sana kurekebisha dalili za msongo wa mawazo.

Zina utajiri mkubwa wa vitamin D. Samaki wana kiwango kikubwa cha vitamin D na inasadikika ni chanzo kikubwa cha virutubisho vingi. Pia vitamin D ina faida calcium ambayo inasaidia afya ya mifupa na ukuaji.

Kuongeza uono na afya ya macho acid ijulikanayo kama omega -3 fatty acids ina faida kubwa ya kuongeza uono na afya ya macho. Sio afya ya macho tu bali pia afya ya ubongo. Hivyo ni muhimu sana.

Ulalaji mzuri kama una tatizo lolote la kupata usingizi, kula samaki zaidi kunaweza kurekebisha hali hiyo. Kula samaki mara kwa mara kunasaidia kuongeza ubora wa usingizi. Wachunguzi wanasema kwamba hii inatokana na samaki kua na vitamin D kwa wingi ambayo inasaidia sana katika kulala vizuri.

Zinasaidia kuondoa chunusi na harara kama una matatizo yoyote ya chunusi zitokanazo na na homoni au ukuaji , samaki zitakusaidia sna kurekebisha ngozi yako. Samaki wana mchango mkubwa sana wa kusafisha na kutunza ngozi.

Zinasaidia kupunguza rheumatoid arthritis (magonjwa ya baridi yabisi) Kama unaumwa ugonjwa huu ambao unasababisha maumivu ya viungo vya mwili, unashambulia tishu za mwili na kuleta maumivu makali ya viungo ni muhimu kula samaki kwa wingi zitasaidia sana kupunguza atahari za ugonjwa huu.

Zinapunguza hatari ya kupata cancer wataalamu wa afya wanaeleza kwamba ulaji wa samaki wa mara kwa mara unasaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya kansa kam vile kansa ya kinywa, kansa ya kongosho na zingine nyingi tofauti na wale wasiokula samaki mara kwa mara.

Zinasaidia kuongeza ufahamu na utulivu andiko moja lilieleza kwamba uchunguzi uliofanyika umebaini kwamba wanafunzi kati ya umri wa miaka 14 – 15 ambao walikula samaki mara kwa mara kuliko nyama wana uwezo mkubwa wa kupata utulivu na uelewa katika masomo yao tofauti na ambao hawali.

Samaki zina madini mengi mbalimbali kama iron, zinc, iodine, magnesium na pottassium hivyo unashauriwa uendelee kula samaki zaidi na vyakula vingine vya jamii hiyo ili kupata afya zaidi ya moyo, ubongo, ngozi na mwili wako kwa ujumla.

Samaki hazina mafuta mengi (low fat) kulinganisha na nyama zingine. Chama kimoja huko America kinachohusika na afya ya moyo (America Heart Association) kilishauri ni muhimu kula angalau samaki mara mbili kwa wiki kama sehemu ya chakula bora (health diet).

Leave a comment